News

Uhuru atofautiana na Pombe kuhusu korona

Maradhi ya korona yamezua tofauti kali kati ya Tanzania na Kenya na yanatishia urafiki na uhusiano mwema kati ya nchi mbili za Afrika Mashariki.

Serikali ya Kenya ikiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta juzi ilitangaza kufunga mipaka yake na nchi jirani ya Tanzania ili kuwalinda raia wake kutokana na maradhi hatari ya korona. Haya yalijiri baada ya serikali ya Kenya kupitia wizara ya afya kusajili takribani visa 23 vya maambukizi ya korona kutoka kwa wasafiri na madereva wa lori kutoka nchi ya Tanzania.

Jambo hili lilimkera sana Rais Pombe ambaye bila kusita ameamua mipaka ya nchi hiyo jirani ifungwe maramoja.
Mkuu wa mkoa wa Arusha .


” Mimi kama mthamini wa mkoa huu, natoa ilani ya kufunga mpaka huu maramoja na kuwataka madereva wote wa Kenya kutoingia Jamhuri ya Tanzania maramoja. Juzi kwenye vipimo vyetu, waKenya kumi na tisa walipatikana na virusi vya korona. Sisi hatutawaruhusu wao kutuletea hizo korona zao huku wakifanya mazingira yetu ya kufanya biashara kuwa magumu . Natoa ilani kuwa yasiruhusiwe hayo magari ya Wakenya lakini kama kuna yale ya kwenda Zambia, Burundi na Kongo yaruhusiwe ila tu yawe yanaendeshwa na raia wa hizo nchi” Mkuu huyu wa mkoa alinukuliwa akisema.

Hali hii huenda ikazua tandabelua na kusisimua mihemko ya kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.

Kwa sasa magari yote ya kuingia Tanzania na kutoka hayaruhusiwi na nchi zote mbili.

Kwa sasa Uhuru bado ametofautiana na Pombe

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button