News

Sitishiki kamwe kwa kubanduliwa Chamani, asema Seneta Malala wa Kakamega

Sitishiki kamwe kwa kubanduliwa Chamani, asema Seneta Malala twa Kakamega

asema Malala

Seneta wa kaunti ya Kakamega Mheshimiwa Cleophas Malala amesema kwamba hajashtuliwa na kitendo cha chama cha Anc ambacho kinaongozwa na Musalia Mudavadi kumtimua chamani.

Mnamo tarehe 25/6/2020 kamati kuu ya chama cha Anc ilitangaza kubanduliwa chamani kwa mwanasiasa huyu wa kaunti ya Kakamega.

Katibu mkuu wa chama hicho Bwana Muluka alisema kwamba seneta huyo wa Kakamega amekuwa na utovu wa nidhamu na kuasi chama ambacho kilimpa tiketi ya kuingia bungeni.

Mwaka jana Seneta Malala alikaidi msimamo wa Chama na kumpigia debe mpinzani wake wakati wa uchaguzi mdogo kwenye eneo bunge la Kibra.

Chama chake kilikuwa kinamuunga mkono Bwana Eliud Owalo dhidi ya Imran Okoth wa Odm.

Jumamosi katika mkutano ulioandaliwa na Gavana Oparanya huko Kakamega, Bwana Malala alisema ya kwamba hajutii na hajatishika kamwe na kitendo cha Anc kumbandua kwenye chama.

“Uongozi hutoka kwa Mungu sio kwa chama. Mimi nilikuwa mtoto wa miaka minne wakati Bwana Mudavadi aliingia bungeni. Inanishangaza kuona leo hii ananipiga kwa mijeledi,nyundo na bunduki. Bwana Mudavadi mimi ni kijana yako” alisema Malala.

Chama cha Anc kimesema hakitalegeza msimamo kwa wale wote wanao mkejeli na kumsuta kinara wa chama hicho.

Bwana Mudavadi yuko mbioni kuwania kiti cha urais mwaka wa 2022.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button