News

Mke wa Shujaa Ronald Ngala Bi Esther Ngala afariki.

Mjane wa aliyekuwa mpiganiaji wa Uhuru Marehemu Ronald Ngala Bi Esther Ngala amefariki.Bi Esther Ngala alifariki leo.

Wakenya mbali mbali wamejumuika na familia ya mwendazake na kuwapa pole wakati huu mgumu.

Katibu mkuu wa chama cha wafanyi kazi Bwana Francis Atwoli alikiwa na haya kusema:

Pole Sana @Katana kwa kumpoteza Mama wetu mpendwa. Marehemu Martin Shikuku alikuwa kila wakati akitukumbusha ukarimu wake Mama Esther. Mungu aiweke roho yake Mahali pema peponi” Daktari Atwoli .

Gavana wa Mombasa Mheshimiwa Joho naye alimuomboleza mama Esther Ngala kama shujaa wa ukombozi wa nchi yetu.
“Nimepokea taarifa ya kifo cha mama Esther Ngala kwa majonzi zaidi. Nilimfahamu marehemu pamoja na mumuwe marehemu Ronald Ngala kama wakereketwa wakubwa wa upiganiaji wa uhuru na kutaka uwepo wa majimbo nchini Kenya. Mola ailaze roho yake mahali pema peponi” Bwana Joho kasema.

Marehemu Esther Ngala na mamaye aliyekuwa waziri hapo awali na mjumbe wa eneo bunge la Ganze Mheshimiwa Noah Katana Ngala.

Esther Ngala atazikwa katika kijiji cha Vishakani Kaloleni mahali ambapo mumewe Ronald Ngala alizikwa 1972

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button